Forgive Assenga anatafuta kazi

---- mwanzo wa ujumbe -----


Je unahitaji mtu wa kupokea na kuchangamsha wateja wako? Naitwa Forgive Assenga, nina miaka 22 na elimu ya kidato cha nne, na ujuzi wa kutumia computer. Kabla hamjanishambulia kwa elimu yangu ndogo si mapenzi yangu bali ni mapenzi ya Mungu baada ya baba yangu kufariki nami nikashindwa kuendelea zaidi. Hata hivyo nina maono ya kujielimisha zaidi, sema kwa maisha ya sasa ni muhimu kufanya work-study la sivyo mambo hayaendi.

Uwezo wangu mkubwa ni kuongea na watu. Huwa siishiwi maneno na mtu yeyote akiwa nami hawezi kuboreka. Naamini naweza kumudu nafasi yoyote inayohitaji uwezo wa kuongea kama vile kutafuta wateja (sales/marketing), au kupokea wateja (receptionist). Ukinipa maelekezo ya kutosha kuhusu kampuni au biashara yako, na kazi husika naweza kuifanya kwa ufanisi tu. Kikubwa ni usichoke kunielekekeza katika miezi mitatu ya kwanza. Baada ya hapo nitakuwa fiti.

Vile vile kwa watu wanaohitaji models wa kuweka kwenye matangazo ya picha sura yangu naamini ina mvuto wa kutosha kuvutia wateja. Hivyo kama unahitaji sura yenye mvuto uweke kwenye tangazo lako tuwasiliane pia.

Asante kwa kusoma maelezo haya. Kwa maelezo zaidi tuwasiliane:

E-mail:
forgive.assenga@gmail.com
Simu: 0713 620 274

Asante na Mungu akubariki,
- Forgive

------ mwisho wa ujumbe ------

tafadhalini wadau, kwa niaba yake na wengine walipo kwenye mazingira kama yake nawasihi mumsaidie... kichwangumu.


Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.