Ratiba ya mazishi ya Hayati Walid Juma


Taratibu za kusafirisha mwili wa Hayati mpendwa wetu Walid Juma kutoka Ufaransa zimeshakamilika na pia ratiba ya mazishi imeshakamilika kwa sasa.  Ratiba kwa kifupi itakuwa kama ifuatavyo,

Mwili unatarajiwa kuwasili na ndege ya KLM siku ya alhamisi saa nne kasoro dakika 20 usiku, utapokelewa JNIA na utapelekwa nyumbani kwa marehu Upanga. Mazishi yatafanyika siku ya ijumaa saa tano mchana katika makaburi ya Kisutu, lakini kabla ya hapo kuanzia saa tatu na nusu watu wataweza kutoa heshima  zao za mwisho pale kwenye viwanja vya Karimjee. 

Tafadhali jitahidi ufike kwa wakati kwani shughuli hiyo inategemewa kuchukua muda mfupi wa saa moja tu.

Kwa sasa dua zetu zote tunazielekeza kwa hayati Walid Juma na kumwombea roho yake ipate pumzika mahali pema pepote. Amina.

RATIBA YA MSIBA WA ALIYEKUWA KAMISHNA WA USHURU NA FORODHA HAYATI WALID OMAR JUMA IJUMAA, 12 OKTOBA, 2012.


TAREHE

MUDA

TUKIO

MHUSIKA
11 Oktoba, 2012
03.40 Usiku
Mwili wa Marehemu Kuwasili Uwanja wa Ndege wa KNIA Cargo ukitokea Ufaransa.

Familia/Mwajiri wake

04.10 Usiku
Mwili wa Marehemu Kuelekea Nyumbani kwake Upanga.

Itifaki
12 Oktoba, 2012
02.00 – 02.30
Mwili wa Marehemu Kuondoka Nyumbani kwake Upanga na Kuwasili Msikiti wa Ibadhi barabara ya Moscow na India.

Itifaki
02.30 – 03.00
Mwili wa Marehemu Kuombewa Msikitini.

Familia/Itifaki
03.00 – 03.30
Mwili wa Marehemu Kuondoka Msikiti wa Ibadhi na kuwasili Viwanja vya Karimjee kwa Heshima za Mwisho.

Mwajiri wake
03.30 – 04.30
Wasifu na Kuaga Mwili wa Marehemu.

Mwajiri wake
04.30 – 05.00
Mwili wa Marehemu kuondoka kwa msafara na kuwasili katika Makaburi ya Kisutu.

Itifaki
05.00 – 05.30
Ibada na kukalimisha Maziko.
Wanafamilia


Comments

bongotambarare said…
Imeniuma sana... Mungu ailaze roho ya Hayati Walid Juma mahala pema peponi, amina.

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.