Mhasibu 'amtosa' Balozi Mahalu

Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,April 24, 2008 @00:10
Habari nyingine
  • Mhasibu 'amtosa' Balozi Mahalu
  • 339 wafukuzwa Mlimani
  • Mwanafunzi wa kike akutwa na risasi mbili
  • Polisi wajipanga ‘kubana’ uhalifu Sullivan
  • Mbaroni kwa tuhuma za kuua mume kwa kisu
  • Wanaoshindwa mtihani kidato cha pili kutorudia darasa
  • Wabunge wanawake wataka uwaziri mkuu
  • Shirika kutowauzia nyumba wapangaji
  • Nguzo za umeme Zuzu hadi Gairo zimeoza
  • Wilaya 40 hazina hakimu wa wilaya
  • ALIYEKUWA Mhasibu katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Steward Migwano, amedai alielekezwa na Balozi Costa Mahalu kuandaa malipo ya Euro milioni tatu kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ubalozi bila ya yeye kuona mkataba wa mauzo.

    Migwano aliyefanya kazi Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kuanzia Januari 2001 hadi Januari 2007 kama mhasibu, alisema alipojaribu kuhoji juu ya mkataba wa mauzo wa jengo hilo, alielezwa na Profesa Mahalu kuwa mkataba huo ulikuwa bado uko kwenye mchakato wa kuandaliwa.

    Migwano, ambaye kwa sasa anafanya kazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kuwa aliandaa malipo ya Euro 3,098,741 kama alivyoelekezwa na Balozi Mahalu pamoja na Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin, ya ununuzi ya jengo hilo.

    “Balozi aliniambia kwa kuwa mkataba unahusisha nchi mbili bado ulikuwa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia kwa kukamilisha taratibu mbalimbali…hivyo nikafanya malipo yake kutokana na barua alizokuwa anafanya balozi na wizara,” alisema shahidi huyo aliyekuwa anaongozwa na Wakili wa Serikali, Ponsiano Lukonsi.

    Migwano alisema hata hivyo baada ya kufanya malipo hayo, alikuja kuona mkataba uliosajiliwa kwenye mamlaka za Italia ambao ulieleza kwa uwazi kuwa ununuzi wa jengo hilo ulifanywa kwa Euro 1,032,912 na siyo Euro 3,098,741 kama alivyoelekezwa na maofisa hao waandamizi wa ubalozi.

    kwa habari zaidi bofya hapo chini
    http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=8495

    Comments

    Popular posts from this blog

    FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

    Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.