Msiba wa Isaac Kwagilwa

Leo saa mbili asubuhi mwili utapelekwa nyumbani kwake sinza mori ukitokea muhimbili na kuombewa sala fupi na heshima za mwisho, baadae saa tatu asubuhi msafara wa kuelekea kanisani st. albans anglican church utaanza.

misa ya kumuombea marehemu na heshima za mwisho itafanyika kanisani hapo, maeneo ya posta mpya kuanzia saa nne asubuhi. baada ya misa ndugu wanaosafiri wataagana na jamaa na marafiki wanaobaki tayari kwa kuanza safari ya kuelekea makuyuni, tanga kwa mazishi kesho jumamosi.

tunawaombea wote watakaoshiriki na hata kusafiri, Mungu awabariki na kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. amen.

Comments

Popular posts from this blog

Taarifa za msiba...

HARUSI YA KAKA YETU ND. MOSES MUDONKO...