Msiba wa Isaac Kwagilwa

Jana jioni ndugu yetu, kaka yetu, baba yetu na rafiki yetu, na mume wa mama yetu mzee isaac kwagilwa aliiaga dunia katika hospitali ya muhimbili jijini dar es salaam. marehemu isaac alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu, wengi wetu tuliomfahamu alikuwa akizidiwa hupata dawa zake na kupumzika kwa muda na hatimaye kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

kwa jana, alijisikia vibaya nyumbani kwake sinza mori opposite na meeda bar. akaondoka kuelekea hospitali na mkewe ili kupata vipimo na hatimaye dawa kama ilivyokuwa kawaida. alipofika muhimbili kwa daktari wake alipata vipimo na dawa, akaruhusiwa kuondoka ili akatumie dawa nyumbani na kupumzika. akiwa njiani kurudi nyumbani na mkewe, hali ikazidi kuwa mbaya, hivyo kulazimika kurudi hospitali.

hapo hospitalini hali haikutengemaa na hatimaye akaiaga dunia. msiba uko nyumbani kwake sinza mori.

taratibu za mazishi zinaendelea tangu jana, na waombolezaji wanazidi kumiminika kutoa pole na rambi rambi zao. kwa taarifa za leo asubuhi mdogo wa marehemu david kwagilwa ataondoka kuelekea makuyuni tanga akiwa na baba wa marehemu kwenda kufanya maandalizi ya mazishi.

tunategemea mazishi yatakuwa jumamosi na safari ya kuelekea tanga makuyuni itaanza ijumaa nyumbani kwa marehemu.

kwa niaba ya wana jumuiya wa blogu na jamaa wote nawapa pole na kuwaombea mke, watoto, na ndugu wote wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

pole zimetoka holland kwa luttu j. nginilla, abraham aziz wa marekani, Nuraiyah wa canada na kwingineko duniani.

tulimpenda sana ngugu yetu isaac kwagilwa ila muumba alimpenda zaidi.

BWANA AMETOA, NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, AMEN.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.